Adhkaar wakati wa kukusanya kati ya swalah mbili

Swali: Kukitokea madhara kwa sababu ya kukusanya ambapo kukakusanywa swalah. Je, kukikusanya kunaswaliwa Raatibah ya Maghrib na ´Ishaa na pia kunasomwa Adhkaar na Maghrib na ´Ishaa au inatosheleza kusoma baadhi yake pasina zengine?

Jibu: Kuhusu hizo Raatibah mbili zinatakiwa kuswaliwa; mtu anaanza na Raatibah ya Maghrib kwanza kisha anaswali Raatibah ya ´Ishaa.

Kuhusu Adhkaar lililo dhahiri ni kwamba mtu atosheke na kusoma Dhikr moja. Lakini ni Dhikr ipi ambayo ni nyingi zaidi ya Maghrib au ya ´Ishaa? Dhikr ya Maghrib. Mtu akisoma hizo tu natumai kuwa ni zenye kutosheleza.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (33) http://binothaimeen.net/content/736