1Nilijifunua kwa watu wale ambao hawakuniulizia.

Nimeonekana na watu wale ambao hawakunitafuta.

Kwa taifa lile ambalo halikuliita Jina langu,

Nilisema: ”Niko hapa, niko hapa.”

2 Mchana kutwa nimeinyoosha mikono yangu

kwa watu wakaidi,

wanaokwenda katika njia ambazo si nzuri,

wafuatao mawazo yao wenyewe:

3taifa ambalo daima hunikasirisha

machoni pangu,

wakitoa dhabihu katika bustani

na kufukiza uvumba juu ya madhabahu za matofali;

4watu waketio katikati ya makaburi

na kukesha mahali pa siri,

walao nyama za nguruwe,

nazo sufuria zao zina mchuzi wa nyama zilizo najisi,

5Wasemao: ”Kaa mbali; usinikaribie,

kwa maana mimi ni mtakatifu mno kwako!”

Watu wa aina hiyo ni moshi katika pua zangu,

ni moto uwakao mchana kutwa.

6Tazama, jambo hili hubakia limeandikwa mbele zangu:

sitanyamaza, bali nitalipiza kwa ukamilifu;

nitalipiza mapajani mwao:

7dhambi zenu na dhambi za baba zenu, asema Bwana.

Kwa sababu walitoa dhabihu za kuteketezwa juu ya milima

na kunichokoza mimi juu ya vilima,

nitawapimia mapajani mwao

malipo makamilifu kwa matendo yao ya zamani.”

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Isaya 61:01
  • Imechapishwa: 18/01/2020