Swali: Asiyetoa zakaah ataadhibiwa kabla ya kuhesabiwa?

Jibu: Ataadhibiwa kabla ya Moto. Ataadhibiwa siku ya Qiyaamah.

Swali: Vipi kuhusu mtu ambaye hatoi zakaah kikamilifu?

Jibu: Atapewa fungu lake la adhabu kwa kiasi alichofanyia ubakhili.

Swali: Baadhi yao wanatoa zakaah ya Ramadhaan iliyopita na inayokuja mbele.

Jibu: Ni sawa akiharakisha kuitoa.

Swali: Vipi kuhusu kuichelewesha baada ya kuzungukiwa na mwaka?

Jibu: Hapana, haijuzu kwake kuchelewesha. Ikishapitikiwa na mwaka basi analazimika kuitoa na asiicheleweshe. Asiicheleweshe.

Swali: Anasema kuwa hayo ndio mazowea yake.

Jibu: Haijalishi kitu. Aachane na mazowea yake mabaya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22772/هل-يعذب-مانع-الزكاة-قبل-ان-يحاسب
  • Imechapishwa: 19/08/2023
Takwimu
  • 321
  • 373
  • 1,819,089