Adhaana za kuchezeshwa hazifai


Swali: Kuna mtu amejenga msikiti na ni mwenye kupenda sauti za baadhi ya waadhini. Kwa hivyo anacheza sauti ya muadhini huyu kunapoingia wakati wa kila adhaana. Je, kitendo chake hichi ni sahihi?

Jibu: Hapana. Si sahihi. Haisilihi. Haijuzu kuachwa akaendelea kufanya kitendo hichi. Adhaana ya muadhini inatosheleza kwa sauti yake hai, na si sauti ya kuchezwa. Adhaana haitakiwi kuchezeshwa. Inatakiwa iwe adhaana ya aliye hai.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (82) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-08-3-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2018