Swali: Katika baadhi ya misikiti adhaana inatolewa kupitia kanda uliorekodiwa. Je, ni jambo limewekwa katika Shari´ah?

Jibu: Hapana. Hii sio adhaana. Kanda sio muadhini. Adhaana ni ´ibaadah ambayo ni lazima itolewe na muislamu ambaye anawajibika juu ya matendo yake. Kanda hauwajibiki juu ya matendo yake. Haisihi kwayo ´ibaadah. Imechezesha sauti tu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (8) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–14340429.mp3
  • Imechapishwa: 26/01/2017