Swali: Nimeona baadhi ya watu pindi wanapomweka maiti kwenye mwanandani basi hutoa adhaana na kukimu juu yake. Je, kitendo hicho ni sahihi?

Jibu: Hii ni Bid´ah. Kutoa adhaana na kukimu ndani ya kaburi ni jambo la uzushi na halifai. Yote haya hayajuzu. Ni mamoja hayo yamefanyika kabla au baada ya kuzika. Yote mawili hayajuzu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/15849/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B0%D8%A7%D9%86-%D9%88%D8%A7%D9%84%D8%A7%D9%82%D8%A7%D9%85%D8%A9-%D8%B9%D9%86%D8%AF-%D8%AF%D9%81%D9%86-%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%8A%D8%AA
  • Imechapishwa: 10/01/2021