Swali: Wakati fulani nina swali (Swalah za) faradhi mimi mwenyewe kwa kutokuwa na Msikiti ulio karibu na mimi. Je, inanilazimu kwangu adhaana na Iqaamah katika kila Swalah au naweza kuziswali bila ya adhaana au bila ya Iqaamah?

Jibu: Sunnah ni wewe uadhini na ukimi. Hii ndio Sunnah. Ama kuhusu uwajibu, kuna tofauti kwa wanachuoni. Lakini aula na bora zaidi kwako ni wewe uadhini na ukimu, kutokana na ujumla wa dalili. Lakini, ni lazima kwako kuswali pamoja na Jamaa´ah (Msikitini)vovyote itavyokuwa, ukisikia adhaana Msikiti ulio karibu nawe, ni wajibu kwako kumuitikia muadhini na kuhudhuria pamoja na Jamaa´ah. Ikiwa husikii adhaana na wala huna Msikiti ulio karibu, Sunnah ni wewe uadhini na ukimu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 03/04/2018