Adhaana na Iqaamah juu ya misikiti ilio njiani

Swali: Kuna mambo ambayo hutokea katika misikiti ilioko njiani. Kunapoingia kundi la watu ndani ya msikiti na ikawa ni msikiti ulioko njiani wanasimamisha swalah ya mkusanyiko wakati wote. Je, kuadhiniwe kwa ajili ya swalah kwa kila ambao wanaingia? Ikiwa adhaana haikuwekwa katika Shari´ah imamu wao akimu juu ya swalah au akimu mtu mwingine asiyekuwa imamu?

Jibu: Ikiwa kundi hili la watu waliohudhuria wameingiliwa na wakati na wako nchikavu ambapo hakukuadhiniwa na wala hawakusikia adhaana, basi wakifika msikitini waadhini na wasimamishe swalah. Kwa sababu nchikavu woa hawakuadhini wala hawako katika hali ya watu wengine kuwaadhinia. Ama ikiwa wakati wako njiani wanasikia adhaana na wakafika msikitini, basi wakimu swalah pasi na kutoa adhaana.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (68) http://binothaimeen.net/content/1530
  • Imechapishwa: 16/02/2020