Adhaana isiyokuwa na faida


Swali: Kunatakiwa kuwa muda kiasi gani kati ya adhaana ya kwanza na ya pili siku ya ijumaa? Kuna wanaofanya kati yake dakika kumi tu na wengine wanafanya zaidi ya saa  moja. Kuna muda maalum uliotengwa?

Jibu: Kunatakiwa kuweko wakati baina yake. Adhaana ya kwanza haina faida ikiwa inafuatiwa na swalah kisha papo hapo wanafika wanaadhini adhaana ya pili, kama inavyofanywa katika misikiti miwili Mitakatifu. Katika hali hii ile adhaana ya kwanza haina faida. Kwa uchache kunatakiwa kuwe nusu saa kati yake. Lengo ni watu waweze kujiandaa na waje kutokea mbali. Adhaana ya kwanza haina maana wala faida yoyote ikiwa inafuatiwa moja kwa moja na adhaana ya pili. Sivyo hivyo alivyofanya ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (13) http://alfawzan.af.org.sa/sites/de
  • Imechapishwa: 01/10/2017