Swali: Wakati wa adhaana ukipita muadhini anatakiwa kuadhini au atosheke tu kwa kukimu swalah?

Jibu: Akiwa ndani ya mji basi akimu swalah tu ili asiwashawishi wengine. Ama akiwa nje ya mji atoe adhaana. Kwa sababu ndani ya mji misiki mingine itakuwa imekwishaadhini.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (07) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/434/434.mp3
  • Imechapishwa: 15/12/2018


Takwimu
  • 25
  • 413
  • 1,821,444