Swali: Imewahi kuthibiti kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliadhini?

Jibu: Hili swali limeshatangulia kuulizwa. Mliuliza kama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliadhini. Sijui. Sijui lolote kuhusu hili.

Swali: Bora ni kuadhini au kuongoza swalah?

Jibu: Wanachuoni wametofautiana. Kilicho dhahiri – na Allaah ndiye anajua zaidi – kuongoza swalah ndio bora zaidi. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye aliongoza swalah. Ni dalili yenye kuthibitisha kuwa uimamu ndio bora zaidi. Aidha imamu anatakiwa kutimiza masharti fulani ambayo hayakuwekwa kwa muadhini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (8) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–14340429.mp3
  • Imechapishwa: 03/01/2017