Swali: Mimi nimeolewa na mwanaume mwenye kuacha swalah mwezi mzima, miezi miwili na haswali mpaka ijumaa. Siku moja nilikataa kulala nae na kukawa kumetokea baina yetu ugomvi ambapo akanitaliki talaka mbili. Nimechanganyikiwa na nachelea tunachokifanya mimi na yeye ni haramu. Naomba unielekeze na uelekeze wanaume sampuli hii pamoja na kuwa baba yangu hayajui yote yaliyopitika.

Jibu: Mwanaume ambaye haswali kabisa, si ijumaa wala swalah zengine, ni kafiri. Katika hali hii si halali kwa mwanamke kubaki nae sekunde hata moja. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ ۖ لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ

“Mkiwatambua kuwa ni waumini, basi msiwarejeshe kwa makafiri; wao si wake halali kwao na wala wao waume hawahalaliki kwao.” (60:10)

Kuhusu mwanaume ambaye wakati fulani anaswali na wakati mwingine haswali naonelea kuwa sio kafiri. Lakini hata hivyo ni mtenda dhambi kubwa.

Katika hali hii ni wajibu kwa mwanamke kuomba kuitengua ndoa. Ikiwa amekata tamaa juu ya kutengemaa kwake bora zaidi kwake ni yeye kuomba kuifuta ndoa. Kwa sababu mtu huyu atakuwa ni athari mbaya kwake yeye na kwa watoto wake pia. Wakiona kuwa baba yao anachukulia wepesi swalah katika kiwango kama hichi nao watafanya hali kadhalika. Tunamuombea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) uongofu, anyooke katika usawa na mke wake abaki pamoja nae katika furaha na mafanikio.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (17)
  • Imechapishwa: 13/12/2017