Achana na Hizbiyyuun


 

Unajisababishia tu matatizo unapokuwa na Ahl-ul-Bid´ah. Bora ni wao kuwa mbali na sisi na sisi tuwe mbali na wao. Usijiaminishe katu na Hizbiy. Wana mambo ya kuchanga-changa. Ni wajinga na vipofu. Sio waaminifu. Wana maoni dhaifu na yaliyopinda. Wana Bid´ah za Khawaarij. Kwa kweli wana makosa mengi. Haikupasi kupoteza muda wako kwa wewe kuwa mbele yake.

Hawastahiki kusikilizwa. Hawana elimu. Hawana msimamo. Hawana uelewa. Hawana umakinifu. Endapo kutakuwa mmoja wao mwenye elimu, basi elimu inakuwa upande mmoja na yeye wamkuta upande mwingine. Hatuwahitajii. Allaah ametutosheleza nao kwa kutupa elimu ya Qur-aan na Sunnah. Haya ninayoyasema juu ya Hizbiy yule, ndio hayo hayo ninayoyasema juu ya vitabu vyake na kanda zake. Huhitajii kitabu wala kanda yake. Hii ina maana ya kwamba jitengeni mbali na Ahl-ul-Bid´ah hata kama watagawa kanda bure iliorekodiwa vizuri na ilio na anwani nzuri: Muhadhara wa Dr. fulani na fulani. Msiichukue. Msiichukue midhali ni ya mtu Hizbiy.

Kwa mfano kanda “Jalsah ´alaar-Raswiyf” wa Salmaan al-´Awdah. Ni makosa mangapi walipata ndani yake! Pamoja na kuwa ni kanda zinazoitwa kikao cha barabarani, yaani kikao cha haraka.

Hali kadhalika kanda “Bahr-ul-Hubb” wa Ibraahiym ad-Duwaysh. Anazungumzia kuhusu wanandoa, matangamano yao, ni vipi mke anatakiwa kumuheshimu na kumtukuza mume wake na mengineyo. Ni makosa mangapi walipata kwenye kanda hii! Mnaweza kuwa mnakumbuka ni nani aliuraddi? Shaykh ´Ubayd al-Jaabiriy? Allaah amjaze kheri.

Hata kama kanda inazungumzia matangamano kati ya wanandoa usisemi kuwa mtu huyu yuko pamoja na wanachuoni na hawaraddi wanachuoni, viongozi na hawachochei watu. Kwa sababu mtu aliyepewa mtihani wa Bid´ah na Hizbiyyah anaweza kuyaficha yote hayo pindi kunapohitajika kufanya hivo.

Ni makosa mangapi yanapatikana kwenye Khutbah za al-Qarniy! Zimekusanywa kwenye kitabu kinachoitwa “al-Misk wal-´Anbar fiy Khutwab-il-Mibar”. Ni makosa mangapi wamepata ndani yake! Hii ina maana kwamba hayana faida. ´Aa´idh al-Qarniy ana kanda ambapo anawasifu manaswara. Alisafiri kwenda Uingereza kutibiwa magoti ambapo akafurahishwa nao.

Kwa hivyo hamuhitajii vitabu wala kanda za Hizbiyyuun.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.com/Dars-14107
  • Imechapishwa: 19/09/2020