Achague yupi katika wachumba hawa?


Swali: Dada huyu anasema amejiwa na wanaume mmoja anayenyoa ndevu, anayevaa Isbaal, msikilizaji muziki na anayetazama musalsal kwa mwanamke ambaye amehifadhi Kitabu cha Allaah na ni mwanafunzi. Je, aolewe nao au atafute wengine kwa kuwa anasema kuwa pengine baadaye wakaongoka?

Jibu: Hapana. Akitubu na kurejea kwa Allaah Tawbah sahihi (olewa naye). Ama kuolewa naye ilihali bado yuko katika hali hii kwa kutarajia pengine akaongoka katika siku za mbele, hapana.

“Atapokujieni yule ambaye mmemridhia Dini na amaana yake, basi muozesheni.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (69) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13888
  • Imechapishwa: 16/11/2014