Swali: Niliitolea zakaah dhahabu ya kuvaa mwaka wa kwanza, wa pili na wa tatu. Halafu nikahisi uvivu kutoa zakaah katika mwaka wa nne na baada ya hapo na nikajiambia mwenyewe ya kwamba mambo haya wanachuoni wametofautiana na hivyo hainilazimu. Je, hivi sasa nalazimika kutoa zakaah juu ya ile miaka ambayo sikutoa?

Jibu: Ni wajibu kwako kutoa zakaah kwa yale yaliyopita. Wewe mwanzoni ulitoa kwa kujengea ya kwamba ni wajibu na kwamba ni faradhi, ni kipi kilichokuzuia kutoa kwa mara nyingine? Je, ulizisoma dalili ambapo mambo yakakuchanganya? Katika hali hiyo utakuwa ni mwenye kupewa udhuru. Ama kule kusikia tu kuwa ni jambo lina tofauti haifai. Mtu kusikia tu kuwa jambo fulani lina tofauti haifai kwake kurudi katika yale maoni ya mwanzo. Mwanzoni alikuwa akionelea kwamba ni wajibu kutoa zakaah. Ni kipi kilichomgeuza? Je, amezirudi dalili za wale wenye kuoenelea kuwa zakaah ni wajibu na wale wenye kuonelea kuwa sio wajibu? Au amesikia tu kuwa ni jambo lina tofauti ambapo akaonelea asitishe na kwamba tofauti ya Ummah ni rehema?[1] Hili ni kosa.

Namwambia dada yetu – Allaah ambariki – ya kwamba ni wajibu kwake kutoa zakaah juu ya yaliyotangulia. Anatakiwa kutambua yeye na wengine ya kwamba zakaah ni ngawira na sio faini na kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kuwa kila mtu atakuwa chini ya kivuli cha swadaqah yake siku ya Qiyaamah. Kuna yeyote katika sisi atadumu kwa ajili ya mali au mali itadumishwa kwetu? Ni wengi ulioje wa matajiri ambao wamekuwa mafakiri! Ni wengi ulioje wa matajiri ambao wamekufa katika ujana wao! Kwa hivyo tunamwambia dada huyu amtake msaada Allaah na acha ubakhili!

الشَّيْطَانُ يَعِدُكُمُ الْفَقْرَ وَيَأْمُرُكُم بِالْفَحْشَاءِ

“Shaytwaan anakutishieni ufukara na anakuamrisheni machafu… ”

Wanachuoni wamefasiri:

“Kwa ubakhili.”

وَاللَّـهُ يَعِدُكُم مَّغْفِرَةً مِّنْهُ وَفَضْلًا

”.. na Allaah anakuahidini msamaha kutoka Kwake na fadhilah.”[2]

Pata bishara ya msamaha, fadhila na chengine kitachokuwa nafasi badala. Toa swadaqah ya mapambo yako. Kwani hakika maandiko yaliyoenea katika Qur-aan na Sunnah – bali kuna maandiko maalum juu ya mapambo – yanafahamisha juu ya uwajibu wa kuyatolea zakaah mapambo.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/12-tofauti-sio-rehema/

[2] 02:268

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthyamiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (39) http://binothaimeen.net/content/887
  • Imechapishwa: 21/06/2020