Abu Twaalib hakuingia ndani ya Uislamu

Swali: Ami yake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakupatapo kuingia katika Uislamu na akafa juu ya ukafiri, pamoja na kutangaa kwake waziwazi juu ya kumtetea Mtume wa Allaah  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Je, haya yanaingia ndani ya Hadiyth:

“Hakika mmoja wenu atafanya matendo ya watu wa Peponi kwa yale yanayowadhihirikia watu… “?

Jibu: Alifanya hivo kwa sababu ya ule udugu, kama ilivyotajwa katika maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ

”Hakika wewe huwezi kumwongoza umpendaye lakini Allaah ndiye anamwongoza mtakaye.”[1]

Abu Twaalib akasema:

“Lau kama si kutukanywa na Quraysh, basi ningeliitamka.”

Bi maana ningeliitamka shahaadah.

Ibn Hishaam ameeleza katika wasifu wake kwamba al-´Abbaas amesimulia kuwa alitamka shahaadah, lakini katika kipindi hicho alikuwa bado hajasilimu na hivyo upokezi wake si wenye kukubaliwa. Kuhusu maneno yake:

Nilijua kuwa dini ya Muhammad

ndio dini bora ya viumbe

Isingekuwa kwa ajili ya lawama na kuogopwa kutukanywa

basi ungeniona ni mwenye kufunguka waziwazi na kukubali[2]

hayapelekei kwamba aliingia katika Uislamu. Alikataa kuingia katika Uislamu, kama ambavo al-Bukhaariy na Muslim walivyopokea kutoka kwa al-Musayyab bin Huzn. Ndugu yetu Qaasim bin ´Abdillaah at-Ta´ziy ametunga kitabu chenye thamani sana ambapo amemraddi Dahlaan kwa jina ”Asnaa al-Matwaalib fiy Islaam Abiy Twaalib”.

[1] 28:56

[2] al-Bidaayah wan-Nihaayah (3/42).

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1337
  • Imechapishwa: 22/02/2020