Alikuwa ni Abu Salamah bin ´Abdil-Asad bin Hilaal bin ´Abdillaah bin ´Umar bin Makhzuum bin Yaqadhwah bin Murrah bin Ka´b.

Alikuwa ni bwana mkubwa na alikuwa ni kaka yake na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kunyonya na binamu kutoka upande wa shangazi yake Barrah bint ´Abdil-Muttwalib.

Ni mmoja katika wale waislamu wa mwanzo kabisa.

Alihajiri kwenda Uhabeshi kisha akasafiri kwenda al-Madiynah.

Alishiriki vita vya Badr na akafa baada ya hapo kwa miezi kadhaa.

Alikuwa an watoto wengi ambao ni Maswahabah kama mfano wa ´Umar, Zaynab na wengineo.

Wakati ilipoisha eda ya Umm Salamah, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamuoa. Alipokea kutoka kwa mume wake Abu Salamah du´aa ya kusema wakati wa kupatwa na msiba. Alikuwa akisema:

”Hivi ni nani bora kuliko Abu Salamah?”

Alikuwa hafikiri kwamba Allaah atampa mwingine mfano wake. Wakati Allaah alipompa bwana wa viumbe, alifurahi mno.

Alikufa akiwa mtumzima, miaka mitatu baada ya Hijrah.

Ibn Ishaaq amesema:

”Yeye ndiye alikuwa wa kwanza kuhajiri kwenda Uhabeshi. Kisha akarudi pamoja na ´Uthmaan bin Madh´uun na akapewa ulinzi na Abu Twaalib.

Walirejea wakati waliposikia kuwa wakazi wa Makkah wamesilimu wakati kulipoteremshwa Suurah ”an-Najm”.

Musw´ab bin ´Abdillaah amesema:

“Umm Salamah Uhabeshi alimzaa Salamah, ´Umar, Durrah na Zaynab.”

Hawa walizaliwa kabla ya Hijrah.

Umm Salamah amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pindi mtapofika kwa maiti, basi msisemi isipokuwa kheri tu. Kwani hakika Malaika huitikia “Aamiyn” kwa yale mnayoyasema.” Akasema: “Wakati alipofariki Abu Salamah nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Niseme nini?” Akajibu: “Sema: “Ee Allaah! Msamahe na tupe badali njema.” Ndipo Allaah akanipa badali bora kuliko yeye – Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[1]

[1] Muslim (919).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (1/150-153)
  • Imechapishwa: 04/03/2021