Abu Hurayrah alichukua haki kutoka kwa Shaytwaan au kwa Mtume (´alayhis-Salaam)?


Swali: Mwenye kutumia hoja [ya kujuzu] kuchukua haki kutoka kwa yeyote kwa Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) wakati Shaytwaan alimponfundisha Aayat-ul-Kursiy na akaichukua hiyo haki kutoka kwa Shaytwaan:

“Amekuamrisha haki ilihali ni muongo.”

Jibu: Huku sio kuifanyia kazi kauli ya Shaytwaan. Ni kuifanyia kazi kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Amesema kweli ilihali ni muongo.”

Mtume ndiye ambaye amesema haya. Amechukua kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na sio kutoka kwa Shaytwaan.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Sharh Zaad-il-Ma´aad (38) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-01-06.mp3
  • Marejeo: Firqatunnajia.com
  • Imechapishwa: 15/11/2014