Abu az-Zur´ah amesema:

Ukimuona mtu anamtukana mmoja katika Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi tambua kuwa ni zindiki. Hayo ni kwa sababu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni haki na Qur-aan ni haki. Waliotunukulia Qur-aan hii na Sunnah ni Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanachokusudia ni kuwajeruhi mashahidi wetu ili waiporomoshe Qur-aan na Sunnah – wao wana haki zaidi ya kujeruhiwa. Isitoshe ni mazanadiki.

  • Mhusika: Imaam al-Khatwiyb al-Baghdaadiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Kifaayah, uk. 97
  • Imechapishwa: 24/01/2019