´Abdul-´Aziyz Aalush-Shaykh kwamba Jamaa´at-ut-Tabliygh si wenye kuafikiana na mfumo wa Mtume (صلى الله عليه وسلم)

Swali 203: Ni yepi maoni yako juu ya yale yanayofanywa na baadhi ya vijana ambapo wanakusanyika na wanatoka kwa ajili ya kulingania katika dini ya Allaah na wanaliwekea hilo kikomo kwa siku tatu, siku arubaini na miezi mine kwa na wamefanya jambo hilo kuwa ndio kanuni ya Da´wah yao? Ni yepi maelekezi yako juu ya jambo hilo?

Jibu: Kulingania kwa Allaah ni jambo linalotakikana na lililokokotezwa. Isitishoe ni tendo jema. Walinganizi wanaolingania kwa Allaah kama wanataka kufaulu kwa Da´wah yao basi mfumo wao uwe wenye kuafikiana na Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yale waliyokuwemo walinganizi wenye kutengeneza baada yake hali ya kuwa ni wenye kuifuata nyayo zao na kupita juu ya mfumo wao.

Kuhusu kuweka kikomo cha utokaji kwa masiku, miezi maalum na mfano wa hayo basi ni jambo linaweza kuwa na hatia ikiwa wanafikiria kuwa uwekaji ukomo huu umewekwa katika Shari´ah na kwamba ni ´ibaadah. Sivyo hivyo. Ama ikiwa ni kwa sababu wanaona kuwa ndio wakati ambao wana nafasi na kwamba ndio ambao unaendana na wakati wao pasi na kuufungamanisha na Shari´ah, hii ndio sehemu inayosemwa vibaya. Ama wakifanya utokaji huu na wakaufungamanisha na siku arubaini au miezi mine na mfano wa hayo ya kwamba eti ndio ´ibaadah na kwamba ni mambo yamechukuliwa kutoka katika Qur-aan na Sunnah, basi hakika mambo hayo ni miongoni mwa waliyoyazua katika dini ya Allaah.

Huu ndio mfumo wa Jamaa´at-ut-Tabliygh – tunamuomba Allaah atuongozo sote. Wanazifungamanisha nafsi zao kwa nyakati kama hizi siku au miezi tatu au siku arubaini au miezi mine au miezi sita. Haya ni makosa.

Lililo la wajibu kwa kila hali ni kufuata Sunnah na kufuata mfumo wa dalili. Inatakiwa kutilia umuhimu katika jambo la kulingania kwa Allaah kabla ya kila kitu na kuweka msingi wa ´Aqiydah na kuufanya uwe imara. Ama Da´wah ilioegemea juu ya Adhkaar na nyuradi za asubuhi na jioni peke yake na mifumo iliowekwa na kupangwa na watu wenye kutiliwa shaka katika hali zao nyingi ambao hawatilii umuhimu kulingania katika Tawhiyd, hawawakumbushi watu kuhusu dini ya Allaah, hawawaamrishi kheri na kuwakataza shari, bali wanachojali ni wao kukusanya tu na mambo ambayo Allaah ndiye anayajua zaidi. Mengi katika mambo hayo hayakuzalisha matunda ya kheri na kuihakiki. Hayo si kwa jengine ni kwa sababu si yenye kuafikiana na mfumo aliokuwemo juu yake Muhammad bin ´Abdillaah, Maswahabah zake watukufu na Da´wah ya watengenezaji wenye kupita juu ya mfumo wake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 417
  • Imechapishwa: 14/01/2020