´Abdul-´Aziyz Aalush-Shaykh kuhusu Jamaa´at-ut-Tabliygh 2

Swali: Je, nitoke na Jamaa´at-ut-Tabliygh kwa kuzingatia ya kwamba sijaona jambo lolote libaya kwao?

Jibu: Inajuzu ikiwa utawafundisha Tawhiyd na elimu ya Kishari´ah. Wao – Allaah Awaongoze – hawajali elimu ya Kishari´ah. Ikiwa utatoka nao kwa sababu ya kuwafundisha, Allaah Anaweza Akawaongoza katika elimu na masomo, jambo ambalo ni zuri.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Buhuuth al-Islaamiyyah (72/78)
  • Imechapishwa: 22/04/2015