Swali: Unamnasihi nini yule mwenye kutoka katika Khuruuj na Jamaa´at-ut-Tabliyh?

Jibu: Watu wanadai kuwa wanatoka kwenda kulingania watu katika Dini ya Allaah na kuwaelekeza. Wanasema kuwa hawamuamrishi wala kumkataza yule anayetoka pamoja na wao. Wanasema kuwa hawampi moyo wala kumuogopesha. Wanasema kuwa inatosha mtu kutoka pamoja nao na kuwaiga na kutarajia tu kwamba Khuruuj hizi zitabadilisha hali ya mtu.

Wanajishughulisha tu na Du´aa za asubuhi na jioni. Hakuna yeyote katika wao ambaye yuko na elimu na uelewa katika Dini. Hawajali hilo. Hawana Baswiyrah na hawatilii umuhimu wowote katika mambo ya ´Aqiydah. Wanakosolewa kwa hili hata kama watakuwa na nia nzuri.

Kutokana na hali hii waliomo na Khuruuj zao zilizowekewa kikomo cha siku arubaini au miezi, haijuzu kwenda pamoja nao ikiwa mtu sio mwanachuoni na elimu na Baswiyrah katika ´Aqiydah ya hakika. Ni lazima mtu awe na sifa hizi ili aweze kuwaelekeza na kuwanasihi na kuwabainishia haki na kuwafanya wakafahamu mambo ya kidini.

Mbali na hayo, sijui asli yoyote ya Khuruuj hizi pasina elimu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Buhuuth al-Islaamiyyah (68/60)
  • Imechapishwa: 22/04/2015