Swali: Baadhi ya watu wanatoa dalili kwamba maandamano yanajuzu kwa maneno ya Allaah (Ta´ala):

لَّا يُحِبُّ اللَّـهُ الْجَهْرَ بِالسُّوءِ مِنَ الْقَوْلِ إِلَّا مَن ظُلِمَ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ سَمِيعًا عَلِيمًا

“Allaah hapendi uovu utajwe hadharani isipokuwa kwa yule ambaye kadhulumiwa. Na Allaah daima ni Mwenye kusikia, Mjuzi wa kila jambo.” (04:148)

Jibu: Hili halihusiani na maandamano, Aayah hii haihusiani na maandamano. Inahusiana na malalamiko. Mwenye kudhulumiwa anashtaki na kutaka haki yake kutoka kwake [mtu huyo aliyemdhulumu], hata kama utamuongelea kwa mtawala na kumshtaki kuwa fulani kanidhulumu, kala mali yangu nk [inajuzu kufanya].

Hili linahusiana na mashtaka na kumueleza mtawala au Qadhi kama kakudhulumu. Halihusiani na maandamano.

Lakini – Subhaan Allaah – baadhi ya watu wanaweka shubuha ilihali ni wajinga. Au anajua lakini ana chuki zake tu. Qur-aan isitumiwe kwa mambo kama haya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13267
  • Imechapishwa: 06/09/2020