Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema ya kwamba Aayah za Qur-aan ni kama muziki na nyimbo?

Jibu: Sidhani kama kuna ambaye anasema hivi. Lakini kuko ambao wanasema Aayah za Qur-aan zina sauti ya aina ya muziki, wakiwa na maana ya kwamba maneno ya Qur-aan ni yenye ladha masikio yanaburudika nazo. Wanakusudia kusema hivi. Lakini wamekosea kwenye taabiri. Lau wasingelitumia taabiri kama hii ingelikuwa ni bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (05) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_05.mp3
  • Imechapishwa: 29/06/2018