Aayah ya “an-Nisaa´” inasapoti talaka pasina sababu?


Swali: Ni ipi hukumu kwa mwenye kutolea dalili Kauli Yake (Ta´ala):

وَإِنْ أَرَدتُّمُ اسْتِبْدَالَ زَوْجٍ مَّكَانَ زَوْجٍ

“Na mkitaka kubadlisha mke mahali pa mke.” (04:20)

ya kwamba talaka inajuzu na kubadilisha mwanamke mwingine hata kama itakuwa ni pasi na sababu?

Jibu: Talaka ikiwa ni pasi na sababu imechukizwa. Kwa sababu kinachotakikana ni ndoa ibaki na kuishi kwa wema. Haya ndio yanayoamrishwa na Shari´ah. Shari´ah inaamrisha kubaki na mke, kuvumilia baadhi ya tabia yake mbovu, kama mlivyosikia. Imechukizwa ikiwa ni bila ya sababu. Upande mwingine ikiwa ni kwa sababu imeruhusiwa [mubaah]:

وَإِن يَتَفَرَّقَا يُغْنِ اللَّـهُ كُلًّا مِّن سَعَتِهِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ وَاسِعًا حَكِيمًا

“Na wakifarikiana basi Allaah Atampa utajiri kila mmoja katika wasaa Wake. Na Allaah ni Mwenye wasaa, Mwenye hikmah.” (04:130)

Wakati wa haja talaka imeruhusiwa na pasi na haja imechukizwa.

Imeharamishwa pale ambapo itakuwa ni talaka ya ki-Bid´ah. Talaka ya Bid´ah imeharamishwa. Baadhi yazo ni kumtaliki mke mara tatu kwa tamshi moja, talaka wakati wa hedhi au talaka wakati wa nifasi. Hizi zimeharamishwa. Talaka wakati fulani imeharamishwa, wakati mwingine imechukizwa na wakati mwingine imeruhusiwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13382
  • Imechapishwa: 28/04/2018