Aayah Kursiy kwa mwenye janaba wakati wa kulala


Swali: Mwenye kutaka kusoma Aayah Kursiy wakati wa kulala ilihali yuko na janaba. Je, inajuzu kwake kufanya hivo?

Jibu: Ima asome kabla ya janaba au aoge kwanza kisha ndio asome. Mwenye janaba hasomi japokuwa Aayah. Lakini akitaka kuisoma basi kabla ya hapo anatakiwa kwanza kutawadha ndio alale.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 19/10/2018