Swali: Ni ipi hukumu ya Sunnah ya Fajr pindi muislamu anapoamka kuswali baada kuchomoza kwa jua? Je, inapendeza kwake kuiswali au ni lazima kwake papohapo kuanza na swalah ya Fajr kasha ndio aswali Sunnah yake?

Jibu: Sunnah kwa muumini ni yeye kutanguliza Sunnah ya Fajr kwa njia ya kwamba aiswali nyumbani kasha atoke kuelekea msikitini. Akifika na kukuta swalah haijaswaliwa basi ataswali Rak´ah mbili za mamkuzi ya msikiti. Hivi ndio Sunnah. Kama hakuswali nyumbani, bali amekuja msikitini, basi ataswali Sunnah ya Raatibah msikitini Rak´ah mbili na inamtosheleza kutokamana na swalah ya mamkuzi ya msikiti. Hapana neno vilevile ikiwa atanuia zote mbili Sunnah ya Fajr na swalah ya mamkuzi ya msikiti. Lakini ikiwa Sunnah hii imempita kwa njia ya kwamba kwa mfano amelala na akaamka baada ya kupambazuka kwa alfajiri, basi ataanza kwa Sunnah ya Fajr kisha ndio aswali faradhi. Hivo ndivo alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya swalah ya Fajr wakati alipopitikiwa na usingizi yeye na Maswahabah zake katika baadhi ya safari.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/377)
  • Imechapishwa: 17/08/2022