Aakhirah atakuwa na mume yupi kati ya hawa wawili?


Swali: Mume akifariki na kisha baada ya eda mke wake akaolewa na mwanaume mwingine atakuwa na yupi siku ya Qiyaamah?

Jibu: Hili liko kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Hatujui mambo ya siku ya Qiyaamah. Hili ni kwa Allaah.

Lakini imethibiti ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu mwanamke ambaye alikuwa na waume wengi ni yupi atakuwa mume wake? Akasema atakuwa kwa yule ambaye alikuwa na tabia nzuri zaidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (66) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13844
  • Imechapishwa: 16/11/2014