99. Uwajibu wa kutendea kazi yaliyotajwa na mtunzi wa kitabu

Ukitendea kazi aliyotaja mtunzi katika shairi hili na ukayaamini kama yalivyotajwa, basi wewe uko katika njia sahihi. Ambaye ataonelea kinyume na yaliyotajwa humu, atakuwa ni katika wakhalifu kutegemea na vile ukhalifu wake ulivyo. Hilo sio kwa sababu ya shairi au mshairi mwenyewe. Hilo ni kwa sababu shairi hili limechukuliwa kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Haina maana kwamba analisifu shairi lake. Ni kusifu yale yaliyomo ambayo yana maana ya Qur-aan na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 202-203
  • Imechapishwa: 13/01/2024