99. Ni lazima kutekeleza wasia wa kumsafirisha maiti?

Swali 99: Baadhi ya watu na khaswa watu wazima wanakuwa ni wenye kueshi ar-Riyaadh kwa muda wa kudumu na kabla ya kufa kwake anaacha anausia azikwe katika mji wake. Mahali hapa panaweza kuwa mbali na ar-Riyaadh kwa zaidi ya 100 km. Wengine wanamswalia ar-Riyaadh na yale maeneo ambayo atazikwa. Je, jambo hili linaafikiana na Shari´ah? Je, inawalazimu warithi kutekeleza wasia huu[1]?

Jibu: Kilichowekwa katika Shari´ah azikwe katika mji wake ikiwa ni mji wa Kiislamu. Haikusuniwa kumhamisha kwenda maeneo mengine. Haiwalazimu warithi kutekeleza wasia wa ambaye ameusia kusafirishwa. Hakuna dalili ya hilo. Isitoshe hayo yanakwenda kinyume na yale waliyopita juu yake Salaf wa Ummah huu. Jengine hilo lina makalifisho.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/220).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 68-69
  • Imechapishwa: 07/01/2022