99. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa kumi wa an-Nisaa´

al-´Ayyaashiy amesema:

“Zaraarah amehadithia ya kwamba Abu Ja´far na Humraan ameeleza kwamba Abu ´Abdillaah amesema kuhusiana na maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَاتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلَّا قَلِيلًا

“Lau si fadhila za Allaah juu yenu na rehema Zake basi hakika mngelimfuata shaytwaan isipokuwa wachache tu.”[1]

“Fadhilah za Allaah ni Mtume wake na rehema Zake ni uongozi wa maimamu.”[2]

 Baada ya ´Aliy maimamu hawakuwa na utawala wala mamlaka yoyote juu ya watu, sembuse Maswahabah na wengineo wanaozungumzishwa katika Aayah hii. Elimu yao haikuenea kwa watu. Hakuna chochote ambacho Raafidhwah wanaeneza juu yao isipokuwa batili ambayo inafichua uongo wa Baatwiniyyah hawa.

[1] 04:83

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/260).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intisaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 146-147
  • Imechapishwa: 03/12/2017