La tatu: Msimamo wetu juu ya Qur-aan tunatakiwa kuiheshimu na kuiadhimisha kwa sababu ni maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Fadhilah za maneno ya Allaah ukiyalinganisha na maneno mengine ni kama mfano wa fadhilah ya Allaah juu ya viumbe Wake. Maneno ya Allaah sio kama maneno ya watu wengine. Bali ni kama fadhilah ya Allaah juu ya waja wake. Ni sifa miongoni mwa sifa Zake (Subhaanahu wa Ta´ala). Ni wajibu kukiheshimu Kitabu cha Allaah, kukiadhimisha na kukitukuza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 131
  • Imechapishwa: 17/12/2018


Takwimu
  • 27
  • 413
  • 1,821,446