98. Uwajibu wa kuamini ´Aqiydah hii mwanzo wa maisha hadi mwisho


Imaam Ibn Abiy Daawuud (Rahimahu Allaah) amesema:

40- Midhali utaendelea daima kuyaitakidi haya

     basi wewe utakuwa katika kheri jioni na asubuhi

MAELEZO

Hii ni hitimisho. Ukiendelea kuyaamini yale yote yaliyomo kwenye shairi hili katika uhai wako wote na mwisho wa uhai wako, basi wewe uko katika kheri duniani na Aakhirah. Ama ukiyaamini kwa kipindi fulani halafu ukayaacha na kuyapuuza, hayatokufaa kitu. Ni lazima uendelee kuonelea ´Aqiydah hii katika maisha yako yote mpaka pale utapokufa. Kuhusu yule ambaye atayaamini mara ya kwanza kisha akajireje kwayo, huyu ataangamia pamoja na wenye kuangamia.