Swali 98: Maiti akiwa mfanyakazi na mhamiaji na familia yake wakaomba asafirishwe, jambo ambalo litapelekea kuyatoa matumbo yake, kupakwa dawa na kuwekwa ndani ya jeneza na kumgarimu mdhamini kiasi kikubwa cha fedha. Je, mdhamini wake amzike pale alipofia na apuuze maombi ya familia yake[1]?

Jibu: Kilichowekwa katika Shari´ah ni kumzika mfanyakazi na wengineo pale walipofia. Akiwa ni muislamu basi atazikwa katika makaburi ya waislamu na wala haijuzu kumsafirisha ikiwa kumsafirisha kutapelekea katika yale yaliyotajwa katika kukatikakatika viungo. Muislamu ni mwenye kuheshimiwa katika hali ya uhai na kufa. Isipokuwa ikiwa kusafirishwa kutapelekea katika mambo yaliyowekwa katika Shari´ah na ambayo yatakosekana asiposafirishwa. Katika hali hiyo hapana vibaya kumsafirisha ikiwa haitopelekea kukatikakatika viungo kukiwemo matumbo yake au sehemu yake.

Mfanyakazi akiwa ni kafiri basi haifai kumzika katika kisiwa cha kiarabu. Bali atasafirishwa kupelekwa nchi nyingine ikiwezekana kufanya hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliamrisha kutolewa makafiri nje ya kisiwa cha kiarabu. Amesema:

“Kusikusanyike ndani yake dini mbili.”[2]

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/218-219).

[2] Ahmad (25820) na Maalik (1651).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 67-68
  • Imechapishwa: 07/01/2022