97. Uwajibu wa kuomba kinga dhidi ya mambo mane

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wakati mmoja wenu anapomaliza Tashahhud [ya mwisho] basi amuombe Allaah ulinzi kutokamana na mambo mane:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ جهنم و من عَذَابِ الْقَبْر ومِنْ فِتْنَةِ الْمَحْيَا وَالْمَمَاتِ وَ مِنْ شرِ[فتنة]الْمَسِيحِ الدَّجَّالِ

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba ulinzi kutokamana na adabu ya Jahannam na kutokamana na adhabu ya kaburi, kutokamana na fitina ya uhai na kifo na kutokamana na [fitina ya] al-Masiyh ad-Dajjaal.”

Kisha ajiombee mwenyewe anachotaka.”[1]

Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiiomba katika Tashahhud yake[2].

Alikuwa akiwafunza nayo Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) kama anavowafunza Suurah katika Qur-aan[3].

[1] Muslim, Abu ´Awaanah, an-Nasaa’iy na Ibn-ul-Jaaruud katika ”al-Muntaqaa” (27). Imetajwa katika ”al-Irwaa’” (350).

[2] Abu Daawuud na Ahmad kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

[3] Muslim na Abu ´Awaanah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 159
  • Imechapishwa: 09/01/2019