La pili: Kumpunguza na kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kufuru vilevile. Kwa sababu Allaah (Jalla wa ´Alaa) ameamrisha kumuadhimisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kumtukuza na kumuheshimu. Amesema (Ta´ala):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيِ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌيَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَرْفَعُوا أَصْوَاتَكُمْ فَوْقَ صَوْتِ النَّبِيِّ وَلَا تَجْهَرُوا لَهُ بِالْقَوْلِ كَجَهْرِ بَعْضِكُمْ لِبَعْضٍ أَن تَحْبَطَ أَعْمَالُكُمْ وَأَنتُمْ لَا تَشْعُرُونَإِنَّ الَّذِينَ يَغُضُّونَ أَصْوَاتَهُمْ عِندَ رَسُولِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ امْتَحَنَ اللَّـهُ قُلُوبَهُمْ لِلتَّقْوَىٰ ۚ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ عَظِيمٌإِنَّ الَّذِينَ يُنَادُونَكَ مِن وَرَاءِ الْحُجُرَاتِ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَوَلَوْ أَنَّهُمْ صَبَرُوا حَتَّىٰ تَخْرُجَ إِلَيْهِمْ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
”Enyi mlioamini! Msitangulize mbele ya Allaah na Mtume Wake na mcheni Allaah! Hakika Allaah ni Mwenye kusikia, mjuzi. Enyi mlioamini! Msipandishe sauti zenu juu ya sauti ya Nabii na wala msiseme naye kwa sauti ya juu, kama mnavyosemezana wenyewe kwa wenyewe kwa sauti za juu, yasije kubatilisha mayendo yenu na hali hamhisi. Hakika wale wanaoteremsha sauti zao mbele ya Mtume wa Allaah, hao ndio wale aliowajaribu Allaah nyoyo zao kwa ajili ya taqwa. Watapata msamaha na ujira mkubwa. Hakika wale wanaokuita nyuma ya vyumba, wengi wao hawatii akilini. Lau wangelisubiri mpaka ukawatokea, bila shaka ingelikuwa ni kheri kwao. Na Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (al-Hujuraat 49:01)
Amesema (Jalla wa ´Alaa):
لَّا تَجْعَلُوا دُعَاءَ الرَّسُولِ بَيْنَكُمْ كَدُعَاءِ بَعْضِكُم بَعْضًا
”Msifanye wito wa Mtume baina yenu kama wito wa nyinyi kwa nyinyi.” (an-Nuur 24:63)
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anatakiwa kuitwa kwa ujumbe kwa kusema “Ee Mtume wa Allaah!”, “Ee Nabii wa Allaah!” Haijuzu kumwita kwa kusema: “Ee Muhamma!” kwa kumtaja jina lake, isipokuwa anatakiwa kuitwa kwa ujumbe na utume ili kumuadhimisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa ajili hii ndio maana Allaah siku zote anamwita kwa jina la ujumbe kwa kusema “Ee Mtume!” na “Ee Nabii!”. Hakumtaja kwa jina isipokuwa katika mazingira ya kuelezea na si katika mazingira ya kuita. Amesema (Ta´ala):
مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ
”Hakuwa Muhammad baba wa mmoja yeyote miongoni mwa wanaume wenu.” (al-Ahzaab 33:40)
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَآمَنُوا بِمَا نُزِّلَ عَلَىٰ مُحَمَّدٍ وَهُوَ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ
”Wale walioamini na wakatenda mema na wakaamini yale aliyoteremshiwa Muhammad, nayo ni ya haki kutoka kwa Mola wake.” (Muhammad 47:02)
Huku ni kuelezea. Ama anapoitwa, basi anaitwa kwa jina la unabii au ujumbe. Hivyo kamwe haitakiwi kusema: “Muhammad amesema… ” Bali badala yake unatakiwa kusema: “Mtume wa Allaah amesema… ” au “Nabii wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema… “ Amesema (Ta´ala):
لِّتُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتُعَزِّرُوهُ وَتُوَقِّرُوهُ وَتُسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا
”Ili mumwamini Allaah na Mtume Wake na mumsaidie na mumheshimu na mumsabihi asubuhi na jioni.” (al-Fath 48:09)
Haya yanarudi kwa Allaah (Ta´ala). Huu ndio wajibu kumfanyia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 130-131
- Imechapishwa: 17/12/2018

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 130-131
Imechapishwa: 17/12/2018
http://firqatunnajia.com/97-ukafiri-juu-ya-mwenye-kumtukana-mtume/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)