97. Maiti akifanyiwa yale yapasayo itafaa kumzika usiku


Swali 97: Je, inafaa kumzika maiti usiku[1]?

Jibu: Inafaa kufanya hivo familia yake wakiweza kumuosha, kumvika sanda na kumswalia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwazika baadhi ya wafu usiku. Yeye pia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alizikwa usiku. Vivyo hivyo as-Swiddiyq, ´Umar na ´Uthmaan wote walizikwa usiku. Hivyo ikapata kujulikana kwamba inafaa kuzika usiku kukitimia yale mambo yaliyowekwa katika Shari´ah.

Kuhusu yale yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya makatazo ya kuzika usiku, wanazuoni wameyafisiri kuwa hapo ni pale ambapo mazishi ya usiku yatapelekea kutotekeleza yale ambayo ni wajibu juu ya haki ya maiti. Kwa ajili hii imethibiti katika “as-Swahiyh” ya Muslim kupitia kwa Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amegombeza mtu kuzikwa usiku mpaka kwanza aswaliwe. Hivyo ikafahamisha kwamba maiti akiswaliwa basi itafaa kumzika usiku.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/213-214).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 67
  • Imechapishwa: 07/01/2022