97. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa nane wa an-Nisaa´

al-´Ayyaashiy amesema alipokuwa akifasiri Aayah:

وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـٰذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا

“Mna nini nyinyi hampigani katika njia ya Allaah na walio wanyonge kati ya wanaume na wanawake na watoto wanaosema: “Ee Mola wetu! Tuondoe kutoka katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu na Tujaalie kutoka Kwako mlinzi na tujaalie kutoka Kwako mnusuraji!”[1]

“Abu Baswiyr ameeleza ya kwamba Abu ´Abdillaah amesema: “Ni sisi.””[2]

Allaah amemtakasa Ja´far na Abu ´Abdillaah kutokamana na upumbavu huu. Wakati fulani wanazusha ya kwamba amesema kuwa wao ndio maimamu. Wakati mwingine wanazusha kuwa amesema kwamba wao ndio mawasii ambao wanajua mambo yaliyofichikana. Mara nyingine wanazusha ya kwamba amesema kuwa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio wanyonge kati ya wanaume na wanawake na watoto.

Aayah inahusu wale waumini wanyonge waliokuwa Makkah. Allaah akawashaji´isha waumini walioko al-Madiynah kutoka na kwenda kupambana Jihaad katika njia Yake na kujitahidi juu ya kuwaokoa wanyonge walioko Makkah. Hili ni jambo linalojulikana. Lakini Raafidhwah hakuna Aayah yoyote katika Qur-aan isipokuwa wanachotaka ni kuipotosha maana yake japokuwa katika kupotosha huko kutakuwa na kuwatweza watu wa nyumba ya kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] 04:75

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/257).