Aayah hii inafahamisha juu ya mambo makubwa yafuatayo:

La kwanza: Ni wajibu kumuheshimu, kumuadhimisha na kumtukuza Allaah (Jalla wa ´Alaa) na kwamba yule mwenye kumtukana Allaah basi anakufuru. Kama walivyosema mayahudi:

الْيَهُودُ يَدُ اللَّـهِ مَغْلُولَةٌ ۚ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا

“Mkono wa Allaah umefumbwa.” [Sivyo hivyo, bali] mikono yao ndio ilivyofumbwa na wamelaaniwa kwa yale waliyoyasema.” (al-Maaidah 05:64)

Pia wamesema vilevile:

إِنَّ اللَّـهَ فَقِيرٌ وَنَحْنُ أَغْنِيَاءُ

“Hakika Allaah ni fakiri na sisi ni matajiri.” (Aal ´Imraan 03:181)

Kadhalika manaswara wamesema:

إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ

“Hakika Allaah ni al-Masiyh mwana wa Maryam.” (al-Maaidah 05:17)

Huku ni kumtukana Allaah (´Azza wa Jall) na ni kumkufuru Allaah (Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 130
  • Imechapishwa: 17/12/2018