96. Sura ya pili: Sababu zilizopelekea katika Bid´ah II


1- Kila ambavo zama zinakwenda na watu wakawa mbali na mapokezi ya ujumbe ndivo elimu inakuwa chache zaidi na ujinga unaenea. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote atakayeishi katika nyinyi basi atakuja kuona tofauti nyingi.”[1]

“Hakika Allaah haikuponyi elimu hivihivi kutoka kwa waja. Lakini anaipokonya elimu kwa kuwafisha wanachuoni. Mpaka pasibakie mwanachuoni yeyote ndipo watu watawachukuwa viongozi wajinga. Watawauliza maswali wafutu bila ya elimu. Basi wao watapotea na kuwapoteza wengine.”[2]

 Hakuna kitachopingana na Bid´ah isipokuwa elimu na wanachuoni. Ikikosekana elimu na wanachuoni ndipo Bid´ah itapata fursa ya kujitokeza na kuenea na kusambazwa na wenye nazo.

2- Mwenye kuipuuza Qur-aan na Sunnah basi atafuata matamanio. Amesema (Ta´ala):

فَإِن لَّمْ يَسْتَجِيبُوا لَكَ فَاعْلَمْ أَنَّمَا يَتَّبِعُونَ أَهْوَاءَهُمْ ۚ وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّنِ اتَّبَعَ هَوَاهُ بِغَيْرِ هُدًى مِّنَ اللَّـهِ

“Na wasipokuitikia, basi tambua kwamba hakika wanafuata matamanio yao. Na nani mpotofu zaidi kuliko yule aliyefuata matamanio yake pasi na uongofu kutoka kwa Allaah?”[3]

أَفَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَـٰهَهُ هَوَاهُ وَأَضَلَّهُ اللَّـهُ عَلَىٰ عِلْمٍ وَخَتَمَ عَلَىٰ سَمْعِهِ وَقَلْبِهِ وَجَعَلَ عَلَىٰ بَصَرِهِ غِشَاوَةً فَمَن يَهْدِيهِ مِن بَعْدِ اللَّـهِ

“Je, umemuona yule aliyeyafanya matamanio yake kuwa ndio mungu wake na Allaah akampotoa juu ya kuwa na elimu na akapiga muhuri juu ya masikio yake na moyo wake na akaweka kizibo juu ya macho yake – basi nani atamuongoa baada ya Allaah?”[4]

Bid´ah ni sehemu ya matamanio yaliyofuatwa.

[1] Ahmad (17184), Abu Daawuud (4607) na tamko ni lake, at-Tirmidhiy (2681) na Ibn Maajah (42).

[2] al-Bukhaariy (100) na Muslim (6737).

[3] 28:50

[4] 45:23

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 186-187
  • Imechapishwa: 07/07/2020