96. Kutenga makaburi ya wanamme na makaburi ya wanawake


Swali 96: Je, inafaa kutenga baadhi ya maeneo ya makaburi kwa ajili ya wanawake na baadhi ya maeneo mengine kwa ajili ya wanamme ili iwe wepesi zaidi kwa watembezi wa makaburi kutambua[1]?

Jibu: Sijui msingi wowote juu ya jambo hili. Kilichowekwa katika Shari´ah ni makaburi yawe kwa ajili ya watu wote. Kufanya hivo kuna wepesi na urahisi. Jengine kitendo hichi ndivo walivopita juu yake waislamu kuanzia zama zake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka hii leo kutokana na ninavojua. Baqiy´ ilikuwa ni yenye kushirikishwa kati ya wanamme na wanawake wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kheri yote inapatikana kwa kufuata mfumo wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah wake (Radhiya Allaahu ´anhum) na wale wataofuata njia yao kwa wema.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/212-213).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 66-67
  • Imechapishwa: 07/01/2022