Download

207-

الله أكبر ، الله أكبر ، الله أكبر سبحان الذي سخر لنا هذا وما كنا له مقرنين ، وإنا إلى ربنا لمنقلبون ، اللهم إنا نسألك في سفرنا هذا البر والتقوى ومن العمل ما ترضى ، اللهم هون علينا سفرنا هذا ، واطو عنا بعده ، اللهم أنت الصاحب في السفر ، والخليفة في الأهل ، اللهم إني أعوذ بك من وعثاء السفر ، وكآبة المنظر ، وسوء المنقلب ، في المال والأهل

”Allaah ni mkubwa. Allaah ni mkubwa. Allaah ni mkubwa. Ametakasika kutokamana na mapungufu ambaye ametuwepesishia haya na tusingeliweza wenyewe kuyadhibiti na hakika kwa Mola wetu tutarejea. Ee Allaah! Hakika sisi tunakuomba katika safari yetu hii wema na kukucha na katika matendo unayoyaridhia. Ee Allaah! Ifanye nyepesi safari yetu hii na fupisha umbali wake. Ee Allaah! Hakika Wewe ndiye unayesuhubiana nami katika safari na mchungaji wa familia yangu.  Ee Allaah! Hakika mimi najilinda Kwako kutokamana na ugumu wa safari, ubaya  wa mtizamo na mgeuko mbaya katika mali na familia.”

Akirudi kutoka safari atasema yaliyotangulia na kuzidisha:

آيِبُـونَ تائِبُـونَ عابِـُدونَ لِرَبِّنا حـامِـدُونَ

”Tunarudi hali ya kuwa tunatubia na tunaabudu na hali ya kuwa ni wenye kumsifu Mola wetu.”[2]

[1] 43:13-14

[2] Muslim (02/998).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 04/05/2020