96. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa saba wa an-Nisaa´

al-´Ayyaashiy amesema:

“Abu Baswiyr amehadithia ya kwamba Abu ´Abdillaah amesema: “Ee Abu Muhammad! Allaah amekutajeni katika Kitabu Chake pale aliposema:

وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا

“Atakayemtii Allaah na  Mtume basi hao watakuwa pamoja na wale Allaah aliowaneemesha – miongoni mwa Manabii na wakweli na mashahiidi na waja wema – na uzuri ulioje kuwa pamoja na hao!”[1]

Mtume wa Allaah ndiye Nabii, sisi ndiye wakweli na mashahidi na nyinyi ndiye waja wema. Jiiteni waja wema kama alivyokuiteni Allaah.”

Huku ni kumzulia uongo mkubwa Abu ´Abdillaah na sidhani hata Abu Baswiyr ambaye ni mwongo mkubwa anaweza kuthubutu uongo mkubwa kama huu.

Mhakiki ameelekeza maandiko haya mawili katika “al-Bihaar”, “al-Burhaan” na “as-Swaafiy”. Haya pamoja na kuwa Raafidhwah hawa wanaamini kuwa Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni makafiri na watadumishwa Motoni milele. Ni upumbavu wa sampuli gani!

[1] 04:69

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intisaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 145
  • Imechapishwa: 02/12/2017