95. Watu walioifanya dini yao kuwa ni pumbao na mchezo


Wanaingia katika haya Suufiyyah ambao wamefanya kuchezacheza, ngoma na nyimbo kuwa ni sehemu katika dini. Wanaita kuwa ni Anaashiyd na Qaswiydah. Wanaziimba na huku wakijikurubisha kwa Allaah. Uhakika wa mambo ni nyimbo na taarabu za haramu. Ni pumbao zilizo za haramu.

Wanaingia vilevile katika haya – nao ni msitari wa kwanza – wale ambao wamepinda katika matamanio na yale yanayopendwa na nafsi zao na wanazipa nafsi zao vile inavyovipenda ijapokuwa vitu hivyo vitakuwa vinaenda kinyume na dalili. Huku ni kuifanya dini kuwa pumbao na mchezo. Wanaingia ndani yake watenda madhambi ambao hawayajali maamrisho ya dini na wanafuata yale yanayopendwa na nafsi na matamanio yao.

Kadhalika wanaingia Suufiyyah wafanya ´ibaadah ambao wameingiza ndani ya ´ibaadah yasiyokuwemo. Bali wameingiza ndani mambo ya ngoma na kucheza ambayo yanapingana nayo. Wameyafanya haya kuwa ni dini na wanaimba Qaswiydah za nyimbo kama wanavyofanya manaswara wanapoimba nyimbo zao. Yote haya ni katika kuifanya dini kuwa ni pumbao na mchezo.