95. Tashahhud ya mwisho na uwajibu wake

Baada ya (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumaliza Rak´ah ya nne alikuwa akikaa katika Tashahhud ya mwisho. Alikuwa akiamrisha ndani yake yale aliyoamrisha katika Tashahhud ya kwanza na akifanya yale anayofanya katika Tashahhud ya kwanza. Isipokuwa tu akikaa Tawarruk[1] ambapo paja lake la kushoto likiwa ardhini na miguu yake yote miwili ikijitokeza kutoka upande mmoja [ambao ni wa kulia]. Akiweka mguu wake wa kushoto chini ya paja lake na chini ya muundi[2] na huku akiuinua mguu wake wa kulia[3]. Wakati mwingine alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaweza kuutandaza[4]. Akikamata goti lake kwa mkono wake wa kushoto ili kujiegemeza kwalo[5].

Amesunisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumsifu kama alivyosunisha katika Tashahhud ya kwanza. Tayari kumeshakwishatangulia katika mlango matamshi mbalimbali ya namna ya kumsifu yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] al-Bukhaariy. Kuhusu swalah ya Rak´ah mbili kama, Sunnah ni kukaa Muftarishan. Upambanuzi huu umeelezwa na Imaam Ahmad, kama ilivyotajwa katika ”Masaa-il-ul-Imaam Ahmad”, uk. 79 ya Ibn Haaniy.

[2] Abu Daawuud, Muslim na Abu ´Awaanah.

[3] al-Bukhaariy.

[4] Muslim na Abu ´Awaanah.

[5] Muslim na Abu ´Awaanah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 157-158
  • Imechapishwa: 08/01/2019