95. Kuna ambao wanaacha kufuata haki kwa kutokutaka kulaumiwa

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Na haya ni masuala ambayo ni makubwa na marefu yanakubainikia ukiyazingatia kwenye maneno ya watu. Utaona mtu mwenye kujua haki na anaacha kuifanyia kazi, kwa khofu ya maisha ya dunia au nafasi au anataka kumpaka mafuta mtu. Hali kadhalika utaona wenye kuifanyia kazi kwa nje na si kwa undani. Ukiwauliza nini wanachoitakidi ndani ya moyo, hawajui. Lakini ni juu yako kufahamu Aayah mbili katika Kitabu cha Allaah.

MAELEZO

Watu wengi wanakataa kufuata haki kwa kuogopa asije akalaumiwa. Sababu nyingine ni kwamba hawataki wazipoteze nafasi na dunia yao. Mtu kama huyu anahitajia kuzisoma hali za watu na azitambue vizuri ili aweze kujua ni nani ambaye ni mnafiki na ni nani ambaye ni muumini mwenye imani safi kabisa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 102-103
  • Imechapishwa: 28/11/2023