95. Du´aa ya kupanda kipando

  Download

206-

بِسْمِ اللهِ، الحَمْدُ للهِ سُبْحَانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ  وَإِنَّا إِلَى رَبِّنَا لَـمُنْقَلِبُونَ الحَمْدُ لِلَّـهِ، الحَمْدُ لِلَّـهِ، الحَمْدُ لِلَّـهِ، اللَّهُ أكبَرُ، اللَّهُ أكْبَرُ، اللَّهُ أكْبَرُ، سُبْحانَكَ اللَّهُمَّ إِنِّي ظَلمْتُ نَفْسِي، فَاغْفِرْ لِي، فَإِنَّهُ لَا يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا أنْتَ

”Kwa jina la Allaah. Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah. “Ametakasika kutokamana na mapungufu ambaye ametuwepesishia haya na tusingeliweza wenyewe kuyadhibiti na hakika kwa Mola wetu tutarejea.”[1] Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah, himdi zote njema ni stahiki ya Allaah, himdi zote njema ni stahiki ya Allaah, Allaah ni mkubwa, Allaah ni mkubwa, Allaah ni mkubwa, kutakasika ni Kwako, ee Allaah, hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu hivyo basi nisamehe, kwani hakuna anayesamehe madhambi isipokuwa Wewe.”[2]

[1] 43:13-14

[2] Abu Daawuud (03/34) na at-Tirmidhiy (05/501). Tazama “Swahiyh-ut-Tirmidhiy” (03/156).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 04/05/2020