95. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa sita wa an-Nisaa´

al-´Ayyaashiy amesema:

“Abu Baswiyr amehadithia ya kwamba Abu ´Abdillaah amesema kuhusiana na Aayah:

وَلَوْ أَنَّا كَتَبْنَا عَلَيْهِمْ أَنِ اقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ

“Na lau Tungeliwafaradhishia waziue nafsi zao.. “

“Bi maana kujisalimisha kwa maimamu.

أَوِ اخْرُجُوا مِن دِيَارِكُم

“ au  watoke katika miji yao… “

Bi maana ikiwa ni alama yenye kuonyesha wako radhi nae.

مَّا فَعَلُوهُ إِلَّا قَلِيلٌ مِّنْهُمْ

“… basi wasingelifanya hayo isipokuwa wachache katika wao… “

Bi maana wale watu wenye kuzozana juu ya ´Aliy.”[1]

وَلَوْ أَنَّهُمْ فَعَلُوا مَا يُوعَظُونَ بِهِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ وَأَشَدَّ تَثْبِيتًا

“Na lau wangelifanya yale waliyowaidhiwa nayo ingelikuwa bora kwao na uthibitisho wa nguvu zaidi [juu ya imani zao].”[2]

Udhahiri inaonekana kwamba anamaanisha neno “imamu”, “wako radhi nae” na “watu wenye kuzozana” yanatoka katika Quir-aan. Vinginevyo ni tafsiri ya ki-Baatwiniy inayomsemea uongo Allaah na Qur-aan. Aayah haifahamisha kabisa juu ya kitu kama hicho.

Halafu isitoshe Mola wa walimwengu na ambaye ni Mwenye huruma mno katika wenye huruma atawafaradhishia Ummah waziue nafsi zao kwa ajili ya imamu huyu aliyezuliwa au kwa ajili ya mtu mwengine asiyekuwa Yeye (Subhanaahu wa Ta´ala)? Kamwe! Huu ni mfano moja wapo juu ya uongo na ukengeushaji wa Baatwiniyyah. Maneno Yake (Ta´ala):

وَلَوْ أَنَّهُمْ فَعَلُوا مَا يُوعَظُونَ بِهِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ وَأَشَدَّ تَثْبِيتًا

“Na lau wangelifanya yale waliyowaidhiwa nayo ingelikuwa bora kwao na uthibitisho wa nguvu zaidi [juu ya imani zao].”

bi maana iwapo watu wangelifanya yale waliyoamrishwa na wakajiepusha na yale ya haramu waliyokatazwa basi ingelikuwa ni kheri kwao kuliko kumuasi Allaah – na si kama anavyodai huyu Baatwiniy.

[1] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/256).

[2] 04:66

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intisaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 144
  • Imechapishwa: 02/12/2017