Imaam Ibn Abiy Daawuud (Rahimahu Allaah) amesema:

ولا تَكُ مِن قوْمٍ تلهوْا بدينِهِمْ

39 – Usiwe ni katika watu waliofanya dini yao ni upuuzi

فَتَطْعَنَ في أهلِ الحَديثِ وتقدحُ

     ukawatukana na kawaponda Ahl-ul-Hadiyth

MAELEZO

Usiifanye dini kuwa ni mzaha na mchezo. Hichi ni kitendo cha wanafiki na watenda madhambi. Ni juu yako kuiheshimu dini na kuyaadhimisha maamrisho yake na watu wake. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema kuhusu wanafiki na watenda madhambi:

اتَّخَذُوا دِينَهُمْ لَهْوًا وَلَعِبًا وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا

“Ambao wameifanya dini yao pumbao na mchezo na ukawadanganya uhai wa dunia.” (07:51)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 197
  • Imechapishwa: 13/01/2024