94. Ni vipi watawekwa watu wawili ndani ya kaburi moja?

Swali 94: Ni vipi watawekwa watu wawili ndani ya kaburi moja[1]?

Jibu: Atatangulizwa yule mbora wao upande wa Qiblah kisha amfuatie yule mwengine anayezidiwa ubora. Kila mmoja katika wao atalazwa ubavu wake wa kulia hali ya kuwa ameelekezwa Qiblah. Hapana neno haja ikipelekea kumzika mwengine wa tatu pamoja nao. Kwa sababu imethibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba siku ya Uhud aliamrisha wazikwe watu wawiliwawili na watatuwatatu ndani ya kaburi moja. Akaamrisha atangulizwe upande wa Qiblah yule ambaye ni mwingi wa Qur-aan katika wao.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/212).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 65-66
  • Imechapishwa: 07/01/2022